MKUU wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, amesema kamati ya ulinzi na usalama haitaruhusu mikutano ya hadhara itakayoombwa na vyama vya siasa wilayani humo.
Pamoja
na uamuzi huo, Kasesela amesema kamati hiyo itawasaka na kuwafikisha
katika vyombo vya dola watu wanaomkashifu Rais Dk. John Magufuli na
viongozi wengine wa Serikali.
“Tuendelee na majukwaa ya utendaji, mipasho ya siasa tupumzike ili tuiache Serikali ifanye kazi zake,” alisema.
Alisema
uchaguzi mkuu mwaka jana umepita kwa kumpata Rais, wabunge na madiwani,
hakuna sababu tena ya kuendelea na mikutano ya kisiasa kila kukicha.
“Kama tunataka mbwembwe za siasa majukwaani, tusubiri uchaguzi wa Serikali za Mitaa au uchaguzi mkuu wa 2020,” alisema.
Alisema hatakuwa na msalia mtume na mtu yeyote awe mwana Chadema au CCM, atakayethubutu kunyanyua
mdomo na kumtusi kiongozi yeyote au mwanachama mwenzeke, atakula naye
sahani moja ili kuheshimiana na kutii mamlaka zilizo madarakani.
Wakati
huo huo, amewataka viongozi wa taasisi mbalimbali za dini ambazo
hakuzitaja kumaliza migogoro yao ya uongozi inayoelekea kuhatarisha
amani ya wilaya.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdala, ameahidi kuzishughulikia changamoto mbalimbali za kimaendeleo wilayani humo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment