Image
Image

Pengo awaasa Mapadre kutambua kuwa kazi waliyonayo ni kubariki na si kulaani.


ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amewataka Mapadre wa Kanisa Katoliki kutambua kuwa kazi waliyonayo ni kubariki na si kulaani.
Pengo alitoa mwito huo jana kwenye misa ya upadirisho kwa mashemasi watatu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
Misa hiyo ilihudhuriwa na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, masista na mapadre mbalimbali pamoja na waumini.
Mashemasi hao waliopewa daraja la upadri ni James Ngonyani, William Sindano na Francisco José ambao wote walipangiwa vituo vya kazi katika jimbo la Dar es Salaam huku Pengo akiwataka wawe tayari kufanya kazi watakapohitajika katika majimbo mengine.
Upadrisho huo umefanya jimbo kuu la Dar es Salaam kuwa na jumla ya mapadri 74 ikiondolewa wa mashirika mbalimbali. Alisema kamwe lisitokee neno la laana kutoka katika midomo ya mapadre bali litoke neno la baraka kwao kwenda kwa waumini.
Aliwataka wawe watu wa kutoa faraja kwa waumini kama ambavyo maagizo ya Mungu yanavyoelekeza.
Awali Askofu Pengo aliwakumbusha pia mapadre kuwa parokia zote ziko katika Jimbo Kuu la Da
r es Saam chini ya Askofu Mkuu na kwamba hakuna parokia ambayo ni ya shirika.
Askofu Pengo alitangaza pia parokia mpya tano ambazo ni Parokia ya Wazo, Mikoroshoni, Tabata Kisiwani, Magole na ya Mbagala Kuu ambazo zimefanya parokia za jimbo hilo kuwa 100.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment