CHAMA
cha Kutetea Abiria Tanzania (Chakua) kimesema hakikubaliani na ongezeko
la tozo ya abiria katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na
nchi jirani cha Ubungo (UBT) iliyoanza Julai mosi mwaka huu.
Akizungumza na gazeti hili jana,
Mwenyekiti wa Chakua, Haasan Mchanjama alisema, kuongezeka kwa tozo
kabla ya kituo kuboreshwa ni kuwaumiza wananchi na abiria wanaotumia
kituo hicho.
“Hatukubaliani na hatujapendezewa na kitendo cha
ongezeko la tozo huku kituo kikiwa hakina huduma za msingi, mantiki ya
ongezeko la tozo inamaanisha huduma za msingi zinapatikana,” alisema Mchanjama.
Alisema licha ya kuongezeka kwa
tozo hiyo bado abiria wanapoingia katika kituo hicho wanalipia huduma
za msingi ikiwemo choo, huku abiria na wananchi wakiendelea kuumia kwa
kukosa sehemu za kupumzika pindi wawapo katika kituo hicho.
“Tunajaribu
kuwasiliana na wadau wengine kuona namna tunaweza kufanya kuhusu
ongezeko hili, tozo katika kituo hicho ilianza muda mrefu lakini hakuna
maboresho yoyote, tunahoji fedha hizo walizipeleka wapi?” alisisitiza.
Hivi
karibuni Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam iliongeza tozo katika
kituo hicho, akizungumza Mkuu wa kitengo cha itifaki na uhusiano wa
Halmashauri ya Jiji, Gaston Makwembe alisema
awali kituo hicho kilikuwa kikisimamia uendeshaji wa shughuli zote za
kituo kwa kutumia Sheria Ndogo ya Mwaka 2004 ya Kituo Kikuu cha Mabasi, hivyo kwa sasa inaanza kutumika Sheria Ndogo ya Mwaka 2009 ambayo imefuta matumizi ya sheria ya Mwaka 2004.
Alisema
sheria hiyo ndogo ya mwaka 2009 inawataka wasindikizaji wote wa abiria
watakaoingia katika kituo hicho kulipia Sh 300 badala ya Sh 200
iliyokuwepo awali.
Home
News
Slider
CHAKUA:hatukubaliani na ongezeko la tozo ya abiria katika kituo kikuu cha mabasi UBUNGO.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment