Mwanamuziki
maarufu wa Marekani Beyonce amewataka wamarekani kufikisha hasira na
mkanganyiko kwa wanasiasa na wabunge wao kufuatia mauaji ya kibaguzi
dhidi ya wamarekani weusi.
Watu maarufu nchini Marekani wamekua
wakielezea hisia zao kuhusu kisa cha hivi karibuni ambapo polisi
walionekana wakimpiga risasi mwanaume mweusi wa kimarekani.
Beyonce
amesema ''sote tuna uwezo wa kuonyesha hasira zetu kwa vitendo'',
akiwataka waMarekani kuwasiliana na wanasiasa wao wilayani na kudai haki
ya kijamii na mabadiliko ya kisheria.
Beyonce alitulia kimya kwa
muda wa dakika moja wakati wa onyesho lake mjini Glasglow jana usiku
kuwakumbuka wamarekani wawili waliouawa kwa kupigwa risasi, na kuweka
majina yao Alton Sterling na Philando Castile kwenye screen kubwa huku
akitoa wito wa kumalizika kwa ''vita dhidi ya walio wachache'' nchini
Marekani.
Mumewe Beyonce Jay Z ametoa wimbo mpya kuhusu ufyatuaji
risasi. Katika wimbo wake wenye miondoko ya rap Jay Z anahoji kwanini
Marekani haibadili sheria yake kuhusu silaha?.
Jumanne picha nyingine
ya video ilijitokeza ambapo polisi wawili wa kizungu walionekana
wakimsukuma chini na kumpiga risasi Alton Sterling mjini Louisiana.
Siku
iliofuatia mkanda mwingine wa video uliorekodiwa moja kwa moja kwenye
Facebook -ulidaiwa kuonyesha athari za kupigwa risasi na polisi kwa
Philando Castile katika gari lake Minnesota.
Matukio haya yamezua mjadala mkubwa juu ya ukatili wa polisi nchini Marekani.
Licha
ya Jay Z wanamuziki wengine wa Marekani kama Chris Brown, Solange
Knowles na Swizz Beatz pia wametoa nyimbo kuhusu mauaji ya kibaguzi
nchini Marekani.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment