Rais Barack Obama wa Marekani amesema anaamini kwamba Uingereza na Umoja wa Ulaya zitasimamia ipasavyo utaratibu wa kipindi cha mpito, baada ya Uingereza kuamua kujitoa kwenye Umoja huo. Katika
mahojiano na gazeti la Financial Times, Obama amesema kujiondoa kwa
Uingereza kunazusha maswali muhimu kuhusu mustakabali wa utangamano wa
Ulaya. Kauli hiyo ameitoa kabla ya mkutano wa kilele wa Jumuiya ya
Kujihami ya NATO unaoanza leo mjini Warsaw, Poland.
Kabla ya mkutano huo, Obama anatarajiwa kukutana na Rais wa Baraza la Ulaya, Donald Tusk, na Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Jean-Claude Juncker.
Pia atakutana na Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron.
Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg amesema leo kuwa jumuiya hiyo itafanya mazungumzo ya kujenga na yenye maana na Urusi na haitaki kurudiwa kwa Vita Baridi
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment