Shirikisho
la soka barani Ulaya limetangaza majina ya wachezaji 10 watakaowania
tuzo ya mchezaji bora Ulaya kwa msimu wa mwaka 2015/2016, majina hayo 10
yametangazwa huku Cristiano Ronaldo akipewa nafasi ya kushinda tuzo
hiyo itakayotolewa Agosti 25 mwaka huu.
Majina hayo 10 yametangazwa
baada ya kufanyika mchujo wa majina ya wachezaji 37 ambao walikuwa
wamependekezwa awali na kupigiwa kura, ambapo UEFA imetaja majina ya
wachezaji 10 waliofanikiwa kuingia katika kumi bora ikiwa majina 27 ya
wachezaji yaliingia katika kinyanga’nyiro hicho.
Majina ya wachezaji
hao kumi ni Gareth Bale – Real Madrid, Gian-luigi Buffon -Juventus ,
Antoine Griezmann - Atletico Madrid, Toni Kroos - Real Madrid , Lionel
Messi -Barcelona, Thomas Müller -Bayern Munich, Manuel Neuer - Bayern
Munich , Laveran Ferreira Pepe - Real Madrid, Cristiano Ronaldo -Real
Madrid, Luis Suarez –Barcelona.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment