Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Burundi Hafsa Mossi ameuawa na watu wasiojulikana mjini Bujumbura.
Bi Mossi, aliyekuwa wakati mmoja Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki katika serikali ya nchi hiyo, aliuawa kwa kupigwa risasi katika barabara ya Gihosha, eneo la Nyankoni.
Mbunge huyo aliwahi kufanya kazi na idhaa ya Kiswahili ya BBC.
Msemaji wa rais wa Burundi Bw Willy Nyamitwe amesema amesikitishwa sana na mauaji ya mwanasiasa huyo.
“Nimesikitishwa sana. Dadangu mkubwa Hafsa Mossi, mwanachama wa @EA_Bunge amefariki, amepigwa risasi na wahalifu. R.I.P #Burundi,” ameandika kwenye Twitter.
Waziri wa mambo ya nje Alain Aime Nyamitwe pia ameeleza kusikitishwa kwake na mauaji hayo.
“Nimehuzunishwa
sana na mauaji ya leo#Bujumburaya Mheshimiwa Hafsa Mossi, na mwanachama
wa#EALA. Ni hasara kuu kwa taifa na#EAC,” ameandika kwenye Twitter.
Kura
ya Brexit ilifichua kiwango kikubwa cha kukosekana kwa usawa katika
jamii ya Uingereza, ambayo May ameahidi kushughulikia na kuugeuza ulingo
wa siasa, kwa kutumbukiza chama chake cha Kihafidhina na chama kikuu
cha upinzani cha Labour katika mtikisiko.
Kiongozi anayekabiliwa na shinikizo
Jeremy Corbyn, ambaye aliyeshutumiwa kwa kushindwa kuwashawishi wapiga
kura wa tabaka la wafanyakazi kuunga mkono uwanachama wa Umoja wa Ulaya,
sasa anakabiliwa na kinyang'anyiro kikali cha uongozi. Hapo jana, Owen
Smith alikuwa mgombea wa pili baada ya mbunge mwenzake Angela Eagle
kujiunga katika katika kinyang'anyiro cha kujaribu kumwangusha
msoshalisti huyo mkongwe.
May wakati huo huo, anatarajiwa kuanza
kutangaza baraza lake la mawaziri baadayae leo, akiwemo waziri wa Brexit
atakayeshughulikia mazungumzo ya Uingereza na Umoja wa Ulaya.
Wanawake wanatarajiwa kuzoa nyadhifa kadhaa kubwa, kwa mujibu wa vyombo vya habari, miongoni mwao ni waziri wa sasa wa nishati, Amber Rudd. Hata hivyo, waziri wa mambo
ya kigeni Philip Hammond, kiongozi aliyefanya kampeni za Brexit, Chris
Grayling, ambaye ni kiongozi wa Wahafidhina Bungeni na Justin Greening,
wa wizara ya maendeleo ya kimataifa wanatazamiwa kubakia na nafasi zao.
Home
Kimataifa
Slider
Hafsa Mossi aliyekuwa Msemaji wa Rais wa Burundi na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashriki auawa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment