Maendeleo
katika njia za ufanyaji kazi pamoja na matumizi ya teknolojia
yanavyokuwa kwa kasi yanaweza kutufanya tuamini tumepunguza maumivu
katika viungo vyetu vya mwili ila si hivyo. Tunatumia magari, mitandao
mbalimbali ambayo vizazi vilivyopita havijawahi kuota kutumia.
Mabadiliko
haya mapya katika maisha yetu yenye msisitizo mdogo katika uimarishaji
wa viungo umechukua hatamu na kuathiri maisha yetu kwa maana mwili wa
binadamu ni ule ule toka miaka milioni iliyopita. Na hiyo inasababisha
kuongeza matukio mengi ya maumivu ya mgongo kwa sababu uti wa mgongo
umekwisha athirika.
Watu wengi lazima wakutwe na maumivu ya uti
wa mgongo walau mara moja katika vipindi vya maisha yao. Sehemu kubwa
inayoathirika katika uti wa mgongo ni sehemu ya chini kabisa na sehemu
ya shingoni kwa sababu sehemu hizo ndizo zina beba uzito mkubwa wa mwili
kila siku.
Sababu nyingine zinazosababisha maumivu ya mgongo ni
kuharibika kwa diski, mgandamizo katika vertebra na kudhoofika kwa
mifupa kutokana na upungufu wa tishu (osteoporosis) kutokana na umri
inaweza kusababisha mgandamizo wa vertebra na kusababisha ufa.
Zipo
zaidi ya sababu 100 zinazoweza kusababisha maumivu ya mgongo upande wa
chini; matukio ambayo yanaweza kusababisha maumivu mgongoni na
yasitambulike. Sababu maalumu ya kuleta maumivu ya mgongo inabaki kuwa
ni kuharibika au kuvunjika kwa sehemu zinazounga uti wa mgongo kutokana
na pozi baya la ukaaji.
Watafiti wameonyesha kuwa ukaaji mbovu
katika viti au sehemu yoyote na kutofanya kazi inayoshughulisha misuli
ya mgongo kunachangia maumivu ya mgongo na hata udhaifu katika uti wa
mgongo.
Maumivu katika mgongo na shingoni ni moja ya sababu za
msingi za wafanyakazi kuchukua likizo maofisini. Asilimia 50 ya
wafanyakazi wanajikuta wakipata maumivu ya mgongo na shingo mara moja
kwa mwaka.
Kwa mujibu wa Dk. Yash Gulati, Mpasuaji Mwandamizi wa
uti wa mgongo na viungo kutoka hospitali za Apollo; Delhi, habari njema
ni kwamba asilimia 75 ya matatizo yote yanayohusisha maumivu ya mgongo
yanaepukika, na asilimia iliyobaki yana epukika, mengine yanatibika na
mgonjwa kurudi katika hali yake ya awali ndani ya muda mfupi.
Baadhi
ya sababu za kwa nini kumekuwa na ongezeko la matukio ya maumivu ya uti
wa mgongo ni kutokana na mabadiliko ya maisha kwa watu wanaoishi
mijini. Wengi huwa wanaanza siku zao kwa kupoteza muda mwingi kwenye
magari.
Kuendesha gari kwa muda mrefu kunapelekea maumivu katika
sehemu ya chini ya mgongo. Kuepuka hilo, siti ya dereva inatakiwa iwekwe
vizuri. Kama kuna uwazi kati ya siti na mgongo wa dereva, uwazi huo
uondolewe aidha kwa kuweka mto au kusogeza kiegemeo cha kiti mbele.
Magoti
yanatakiwa yawe juu kidogo. Hiyo inaweza kuwa hivyo iwapo utajaribu
kusogeza kiti mbele au nyuma. Kama upo uhitaji wa kuendesha gari muda
mrefu kama sehemu ya kazi, ni vyema kuendesha kupata mapumziko mafupi
ya kushuka na kujinyoosha na kisha kuendelea na safari. Wakati wa
kushuka ni vyema mguu uanze kufika chini na sio kuruka.
Sababu
kubwa ya pili iliyogundulika katika kuleta maumivu mgongoni ni hizi kazi
za kukaa kwenye kiti muda mrefu (white-collar job) ambazo wafanyakazi
wanapoteza muda mwingi mbele ya kompyuta, hawakai katika viti vile
ipasavyo au wakati ofisi ina samani zinazoathiri ukaaji wa wafanyakazi.
Ni
vyema kila mfanyakazi ahakikishe kiti chake kipo katika kimo
kinachoendana na meza yake ili kutoumiza mgongo. Kompyuta ziwe katika
umbali unaofaa ili kuepuka mtu kukunja mgongo ili aweze kusoma au
kuandika chochote katika kompyuta.
Uzito uliozidi kutokana na
kutofanya mazoezi kunaweza kupelekea maumivu ya mgongo pia. Kwa mujibu
wa Dk. Yash Gulati, uzito uliozidi unapoleta kitambi mara nyingi
hupelekea kujikunja kwa mgongo na kuanza kuleta maumivu katika viungo na
maungio katika mgongo. Ni muhimu sana kwa kila mtu kuhakikisha ana
uzito sawia na urefu wake, ili kupunguza madhara ya kuathiri uti wa
mgongo.
Sababu nyingine inayotokea mara kwa mara ya maumivu ya
mgongo ni kusogea au kuharibika kwa diski alisema Dk. Yash Gulati wa
Hospitali za Apollo;Delhi. Hii inatokea pale ganda la nje la diski
lililo kama shokomzoba katikati ya mifupa miwili ya
vertebral,linapochanika na kusababisha uvujaji wa ute mwepesi uliopo
ndani.
Kulingana na sehemu diski ilipo, inaweza kubana neva za
uti wa mgongo na kupelekea maumivu makali na kupooza kwa miguu na
mikono. “asilimia tisini ya wenye tatizo la diski kuharibika wanapewa
huduma kwa njia maalumu ya mazoezi ya viungo (physiotherapy) na
mapumziko ya kutosha. Ni mmoja kati ya kumi watakao hitaji upasuaji
mdogo (discectomy) wa kuitoa ile diski iliyosogea na kubana neva”
alisema Dk. Gulati.
Apollo ni moja ya hospitali chache
zilizofikia kiwango cha juu cha ubora wa matibabu na kufurahia matunda
ya katika eneo adimu la upasuaji katika uti wa mgongo. Upasuaji wa
kuondoa diski unafanyika kwa kuchukua tahadhari kubwa ya kupunguza
madhara ambayo mgonjwa anapona mapema bila uvimbe mkubwa na pia kuweza
kuendelea na kazi zake za kawaida.
Imetolewa na: Dk. Yash Gulati, Mpasuaji Mwandamizi wa uti wa mgongo na viungo kutoka hospitali za Apollo; Delhi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment