Akifungua
mafunzo hayo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein
Mwinyi ameeleza kuwa kutokana na mabadiliko ya vyanzo vya migogoro
katika jamii ya kimataifa, majeshi ya ulinzi nayo hayana budi
kuwaendeleza askari wake uwezo wa kukabiliana nayo ili kudumisha amani.
“Zamani tulikuwa tunajipanga kulinda mipaka yetu na kufanya maandalizi ya vita na yeyote atakayetushambulia.
Hali
imebadilika sasa hivi. Uharamia, ugaidi na dawa za kulevya ndiyo tishio
la usalama kwa nchi nyingi duniani,” amesema waziri huyo.
Amesema
kutokana na makosa hayo kutekelezwa kwa mitandao mikubwa duniani
yanahitaji ushirikiano baina ya wadau mbalimbali ndani ya jamii ambao
wataunganisha nguvu, ujuzi na uzoefu ili kupunguza kama si kutokomeza
kabisa athari zake.
Dk Mwinyi amesema juhudi za Serikali nyingi duniani kukabiliana na uhamishaji wa binadamu
pamoja na uharamia umesababisha hasara kubwa ambazo zinahitaji mikakati
imara itakayohakikisha biashara na maisha kwa ujumla yanastawi pasipo
kikwazo chochote kutoka kwa watu wachache.
Amesema
hayo mbele ya maofisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu, Shirika la Umoja
wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na Umoja wa Afrika (AU).


0 comments:
Post a Comment