Rais
Paul Kagame wa Rwanda amesema nchi za Afrika ya Mashariki zinapaswa
kujizatiti katika uzalishaji wa bidhaa zenye ubora ili kuinua soko la
bidhaa zinazozalishwa katika ukanda huo na kuzifanya zipate soko nje ya
nchi hizo.
Rais
Kagame amesema hayo wakati akifungua maonesho ya 40 ya biashara ya
kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu
Julius Nyerere na kuongeza kuwa uwezo wa kuzalishwa bidhaa bora katika
ukanda wa nchi za Afrika ya Mashariki upo.
Naye
rais wa Tanzania Mhe.Dr.John Pombe Magufuli amesema ataendelea kuhimiza
wakazi wa nchi za Afrika ya Mashariki umuhimu wa nchi zao kuwa vinara
wa uzalishaji wa bidhaa za ndani ili kuimarisha uchumi wa nchi zao.
Ufunguzi
rasmi wa maonesho hayo ya 40 ya kimataifa ya biashara ya Dar es Salaaam
umeenda sambamba na kutoa zawadi kwa mabanda ambayo yamefanya vizuri
kwa mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment