JESHI
la Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limekana kuwa kuna watu
waliovunjwa miguu waliopo kwenye chumba cha watuhumiwa kilichopo kituoni
na kusema anayetakiwa kusema kuwa kuna watuhumiwa waliovunjwa miguu au
mikoni ni daktari, anaandika Josephat Isango.
Simon Sirro, Kamanda wa
Polisi kanda maalumu ameliambia MwanaHALISI Online kuwa katika chumba
cha watuhumiwa kituoni humo hana taarifa kama kuna watu waliovunjwa
miguu na kama wapo jeshi la polisi huwa linawapeleka kwenye matibabu.
MwanaHALISI
online lilitaka kupata ufafanuzi ikiwa hao watuhumiwa wanapata haki ya
kupata matibabu na kwanini hawafikishwi mahakamani kwa kipindi kirefu
vile kinyume na sheria za nchi zinavyoelekeza wajibu wa polisi kwa
watuhumiwa.
Sirro alipoulizwa kuhusu baadhi ya watuhumiwa kukaa muda
mrefu bila kufikishwa mahakamani, alianza kuongea na simu nyingine na
kukata ya mwandishi aliyekuwa na shauku ya kutaka kujua hatima ya hao
watuhumiwa.
30 June mwaka huu akizungumza waandishi wa habari baada
ya kuachiwa kwa dhamana, katika mahakama ya Kisutu, Tundu Lissu
Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) aliwataka
watetezi wa haki za binadamu na mawakili kupaza sauti ili haki za hao
watanzania ziweze kutambuliwa.
Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida
Mashariki (CHADEMA) aliwataja Abdalah Bushiri, na Adnani Mohamed Mrutu
kutoka Same ambao wamevunjwa miguu na wanateseka katika chumba hicho
bila kufikishwa mahakamani au kupelekwa kwenye matibabu.
“La Pili ni
juu ya wale niliowakuta kule shimoni, na nilioshinda nao usiku wa
kuamkia leo, pale Central kuna watu wamekaa wengine wiki mbili, wengine
wiki tatu, na wengine mwezi, kinyume na sheria ya Tanzania inavyoelekeza
kuwa mtuhumiwa afikishwe mahakamani ndani ya saa 24, isipokuwa kama ni
Jumamosi na Jumapili ambazo sio siku za kazi” alisema Lissu.
“Nilipokuwa
ndani, nimeshuhudia mengi na kweli siku hiyo polisi walikuwa wanahaha,
kamanda wa polisi ametutembelea zaidi ya mara 3 kwa usiku huo”
alisisitiza Lissu.
Lissu alilala mahabusu ya polisi baada ya kuhojiwa
na kunyimwa dhamana ambapo siku moja alifikishwa mahakamani na kusomewa
shitaka la uchochezi katika mahakama hiyo.
Kesi yake inasikilizwa na
Hakimu Yohona Yongolo ambapo kwa upande wa mashitaka, unawakilishwa na
Benard Kongolo, wakili wa serikali mkuu huku Lissu akitetewa na jopo la
mawakili zaidi ya kumi wakiongozwa na Michael Ngalo akisaidiwa na Peter
Kibatala.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment