Kansela Merkel amkaribisha Theresa May Berlin.
Kansela
Angela Merkel wa Ujerumani amesema amemualika waziri mkuu mpya wa
Uingereza Theresa May kwa mazungumzo mjini Berlin, na kuelezea matumaini
ya ushirikiano mwema kati ya Uingereza na Ujerumani. Akizungumza na
waandishi wa habari katika mji mkuu wa Kyrgyzstan, Bishkek mapema leo,
Bi Merkel amesema kuna changamoto nyingi duniani ambazo zinaufanya
ushirikiano huo kuwa wa lazima. Kansela Merkel amesema alizungumza na
Waziri Mkuu May Jumatano jioni, akikataa hata hivyo kusema chochote
kuhusu uteuzi wa Boris Johnson, mpinzani mkubwa wa Umoja wa Ulaya, kuwa
waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uingereza. Ofisi
ya waziri mkuu wa Uingereza imetangaza kuwa Theresa May alizungumza kwa
simu na Kansela wa Ujerumani na rais wa Ufaransa Francois Hollande, na
kuwaeleza kuwa nchi yake inahitaji muda wa kutosha, kabla ya kuanza
mchakato wa kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.
0 comments:
Post a Comment