Waziri
mpya wa fedha wa Uingereza, Philip Hammond, amesema nchi yake haihitaji
bajeti ya dharura, na kwamba badala yake atafuatilia kwa makini hali ya
uchumi mnamo majira ya kiangazi, kabla ya kufanya uamuzi juu ya
matumizi kama kawaida mnamo majira ya mapukutiko.
Hammond
alibadilishiwa kazi na waziri mkuu mpya Theresa May jana Jumatano,
kutoka Waziri wa Mambo ya Nje na kufanywa Waziri wa Fedha. Amesema
atafanya mazungumzo na Gavana wa Benki Kuu ya Uingereza hii leo, na
kutathmini kwa pamoja hali ya uchumi wa nchi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment