Maelfu ya wananchi wakiwemo viongozi wa serikali na wa siasa wamejitokeza kumzika aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kilindi mkoani tanga marehemu Beatrice Shelukindo yaliyofanyika nyumbani kwao kata ya Olorieni jijini Arusha.
Miongoni
mwa viongozi waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na waziri wa afya Mh
Ummy Mwalimu,waziri mkuu Mstaafu Mh Edward Lowassa,wabunge na pia
viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini.
Wengine
ni pamoja na Rais wa mahakama ya afrika Jaji Agustino Ramadhani,msemaji
wa Chama cha Mapinduzi mh Christopher olle sendeka na wakuu wa mikoa na
wilaya mbalimbali ambao wamemwelezea marehemu beatrice Shekukindo kama
kingozi wa mfano.
Marehemu
Beatrice Shelukindo ambaye ameacha mume na watoto watatu alikuwa
mwanasiasa aliyeshika nyadhifa mbalimbali ikiwemo ya Ubunge wa Jimbo
Kilindi 2005-2015 na Ubunge wa Bunge la afrika Mashariki 2001-2004.
0 comments:
Post a Comment