Na,Devotha Songorwa,Morogoro. ..................................................................................................................................
Machinjio
ya Manispaa ya Morogoro yameendelea kuwa kero kwa Wafanyabiashara na
wakazi wa eneo hilo kutokana na kutiririsha maji taka kwenye mitaro ya
maji ya mvua kwa muda mrefu.
Wafanyabiashara hao, Bi.Mushi
Ally na Dismas Layoze wamesema machinjio hayo yamekuwa kero kwao na
hata wapita, njia kutokana na harufu kali inayotokana na maji taka
kutoka machinjioni kutiririshwa na kuingia kwenye mifereji ya maji ya
mvua kando ya barabara iendayo mjini kutoka Msavu.
Wamesema hali hiyo ipo kila siku na kusababisha eneo hilo kuwa na mazingira machafu, hivyo kuwa tishio la kuwepo kwa magonjwa mlipuko ukiwemo ugonjwa wa kipindupindu.
Aidha
wamesema wameiomba idara ya afya manispaa ya Morogoro kulishughulikiea
suala hilo, ili kulinda afya ya wananchi wanaoishi na kufanya biashara
zao katika eneo hilo.Like ukurasa wetu wa Facebook,Instagram,Twitter,kupata habari zinapotufikia.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment