Na. Devotha Songorwa,Morogoro.
.................................................................................................................................
Wananchi wa mkoa wa Morogoro wametakiwa kuendelea kuchukuwa tahadhari ya kutunza mazingira ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko.
Mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya Morogoro FRANK JACOB ameiambia akizungumza na Tambarare Halisi amesewma kuwa ugonjwa wa kipindupindu bado upo, hivyo wakazi wa Morogoro waendelee kuchukuwa tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.
JACOB amesema kuwa takwimu walizozifanya zinaonesha kuwa July 25 mwaka huu, kuna wagonjwa Nane wanaoendelea na matibabu ambapo wagonjwa 6 kati yao wamelazwa katika kituo cha sabasaba, mmoja kituo cha Gwata na mwingine amelazwa kwenye kituo cha Mkono wa Mara na kwamba hakuna aliyeripotiwa kufariki dunia.
Ametaja baadhi ya maeneo ambayo bado yanaripotiwa kuwa na ugonjwa huo kuwa ni Tungi, Mafisa, Mwembesongo, Ngerengere na Kingolwira na kwamba ni kutokana na maeneo hayo kupitiwa na mto Ngerengere, na wakazi wake kutumia maji hayo yasiyo safi na salama.
Aidha JACOB amewataka wananchi kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu kwa kutumia maji safi na salama kwa kuyachemsha, kuweka dawa ya kuulia wadudu ya watergurd, kufanya usafi binafsi, kunawa mikono kabla na baada ya kula, kunawa kwa maji yanayotiririka, kula vyakula vya moto, kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazma na utupaji salama wa taka .
Mganga huyo mkuu wa hospitali ya mkoa wa Morogoro amewataka wakazi wa Morogoro kuzingatia kanuni za afya na kuacha kuishi kwa mazoea, na badala yake wazingatie elimu inayotolewa na maafisa afya wa ngazi zote za serikali, kwa kuwa ugonjwa huo unaepukika.
Like ukurasa wetu wa Facebook,Instagram,Twitter,kupata habari zinapotufikia.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment