Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke
wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao
kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo jijini Dar es salaam Julai 28, 2016.
.................................................................................................................
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Halmashauri ya wilaya ya
Temeke kuondoa wafanyakazi wa mkataba kwa anjia ya kuwapa ajira ya
kudumu kwa wenye sifa na kuwaondoa wasiokuwa na sifa ifikapo Julai 30
mwaka huu. Amesema kitendo cha kutowaajiri na kuwatumikisha
kwa mikataba kwa muda mrefu kinasababisha wakose stahiki zao jambo
ambalo si halikubaliki.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Julai 28, 2016) wakati akizungumza
na watumishi wa halmashauri hiyo na kusisitiza kwamba ni lazima sula
hilo lishughulikiwe haraka kwa sababu hayo ndio matundu watumishi hewa. “Mnawatumikisha
watu kama vibarua kwa muda mrefu, hapa kuna wengine wanafanya kazi kwa
mikataba kwa miaka mitano hadi sita hii haikubaliki kwani mnawakosesha
stahili zao pale mnapowaachisha kazi,” amesema.
Awali
Kaimu Ofisa Utumishi wa Manispaa hiyo Zaitun Hassan alisema wamekuwa
wakitoa ajira za mikataba kwa sababu wamekosa watu wenye sifa za kuweza
kuajiriwa husan madereva. “Kwa mara ya mwisho umetangaza lini
nafasi za ajira? Katika mkoa wa Dar es Salaam kweli wanaweza kukosekana
madereva wenye sifa za kuajiriwa? Alihoji Waziri Mkuu.
Zaitun
alisema kuwa madereva wengi wanaojitokeza pindi wanapotangaza ajira
wanashindwa kufikia vigezo ikiwemo kuwa na cheti cha VETA na badala yake
wanakuwa na cheti cha kidato cha nne tu. Hata hivyo, Waziri
Mkuu amesema kuwa kuna wafanyakazi wengine katika Idara ya Uhasibu na
Ujenzi ambao nao wameajiriwa kwa mkataba hivyo amemtaka Ofisa Utumishi
kuomba kibali cha kuajiri kwa Katibu Mkuu Utumishi.
Katika
hatua nyingine Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda kufanya tathmini ya maeneo yote ya shule kwenye mkoa wake
na watakaobainika kuingia katika maeneo hayo waondolewe haraka. Amesema
baada ya kukamilisha utengenezaji wa madawati kinachofuatia sasa ni
ujenzi wa vyumba vya madarasa, ambapo amezitaka halmashauri kuweka
mipango ya kujenga majengo ya madarasa ya ghorofa ili waweze kuwa na
madarasa mengi katika eneo dogo.
Awali
Waziri Mkuu alipokea msaada wa madawati 705 katika hafla iliyofanyika
kwenye viwanja vya shule ya msingi Chamazi wilayani Temeke ambapo kati
yake Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania umetoa madawati 600 na Jumuia ya
Mabohora imetoa madawati 105. Pia Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dk. Agustino Mahiga alimkabidhi
Waziri Mkuu hundi ya sh. milioni 85 fedha zilizochangwa na watumishi wa
wizara hiyo kwa ajili ya kuchangia utengenezaji wa madawati.
Dk.
Mahija alisema watumishi hao walichanga sh. milioni 100 kwa ajili ya
utengenezaji wa madawati ambapo sh. milioni 15 wamekabidhi kwa mkuu wa
wilaya ya Manyoni Geofrey Mwambe ambaye alikuwa mtumishi wa wizara hiyo
ili naye akatengeneze madawati kwa shule za wilayani kwake.
Kwa
upande wake Balozi wa Kuwait nchini Jaseem Al Najem amesema Serikali ya
Kuwait itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika shughuli
zote za maendeleo hususan katika sekta za elimu na afya.
Home
News
Slider
MAJALIWA atoa siku moja kwa Halmashauri ya wilaya temeke kumaliza tatizo la ajira za mikataba.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment