Image
Image

Magufuli atengua uteuzi wa Mwenyekiti TIB amteua Prof.Palamagamba kuchukua nafasi hiyo.

            Prof. William Lyakurwa. Mwenyekiti wa  TIB ametengua uteuzi.
  Prof. Palamagamba J. A. M. Kabudi-Ameteuliwa kwa  Mwenyekiti wa  TIB 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa mamlaka  aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha sheria ya tafsiri za sheria  (Interpretation of Laws Act )   Sura 1, leo tarehe 5 Julai, 2016 ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB  Prof. William Lyakurwa.
Kufuatia hatua hiyo, kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 9 (2) cha ya Sheria ya mashirika ya umma  (Public Corporations Act ) Sura 257, Mhe. Rais amemteua  Prof. Palamagamba J. A. M. Kabudi kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB kwa kipindi cha miaka mitatu.
Kufuatia mabadiliko hayo, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango  kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha sheria ya sheria ya tafsiri za sheria  (Interpretation of Laws Act )   Sura 1,  ametengua uteuzi wa Wajumbe Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB. Aidha,  kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 9 (1) cha ya Sheria ya mashirika ya umma  (Public Corporations Act, Sura 257) Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango ameteua wajumbe wapya wa Bodi wafuatao kwa kipindi cha miaka mitatu:
1.    Brig. Gen (Rtd) Mabula Mashauri
2.    Dkt. Razack B. Lokina
3.    Bi. Rose Aiko
4.    Prof. Joseph Bwechweshaija
5.    Bw. Said Seif Mzee
6.    Dkt. Arn
old M. Kihaule
7.    Bw. Maduka Paul Kessy
8.    Bw. Charles Singili
Uteuzi  wa Mwenyekiti na Wajumbe wapya wa Bodi unaanza tarehe leo 5 Julai, 2016.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es sa
laam
05 Julai, 2016.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment