Kansela
wa Ujerumani Angela Merkel amesema kwamba Umoja wa Ulaya
utaendelea kukua hata bila ya Uingereza.
Akizungumza katika mkutano
kujadili ujumuisho wa mataifa ya Balkan magharibi , Merkel
alisema kitu pekee ambacho ni muhimu ni kwa mataifa yanayotaka kujiunga na Umoja wa Ulaya kutimiza orodha ya masharti
yaliyokubalika hapo kabla.
Uamuzi wa Uingereza kujitoa kutoka
Umoja wa Ulaya umeleta kiwingu kuhusiana na Umoja wa mataifa
hayo 28 wanachama. Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamejibu uamuzi wa
Uingereza kujitoa kwa kutoa wito wa ufanisi zaidi na umoja
katika Umoja huo.
Wakati baada ya Waingereza waona Umoja wa Ulaya umeingilia uhuru wao, mataifa ya Balkan yanaona kundi hilo
la mataifa kuwa ni chanzo cha uthabiti wa kisiasa na mafanikio ya
kiuchumi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment