Katika
majira ya joto, watu husikia hasira au kuwachokoza wengine mara kwa
mara hivyo mioyo yao inaweza kudhurika. Matibabu ya kichina yanasisitiza
kwamba katika majira ya joto, watu wanatakiwa kuzingatia afya ya moyo
wao. Kwa hiyo tutaandaaje maisha yetu kwa ajili ya kujenga afya ya mioyo
yetu?
Kwanza ni kufanya mazoezi ya mwili asubuhi, lakini usifanye
mazoezi mara moja baada ya kuamka bali kunywa kikombe kimoja cha maji
halafu fanya mazoezi kidogo na lazima ukumbuke kuwa usifanye mazoezi
kupita kiasi.
Pili ni kulala kidogo adhuhuri baada ya kula chakula
cha mchana, unaweza kuamua kulala wakati wa saa tano hadi saa saba
mchana ambao ni wakati unaofaa zaidi kwa kulinda afya ya moyo wako.
Aidha kulala kidogo mchana pia kunaweza kukusaidia kupunguza hatari ya
kupata ugonjwa wa moyo, na hata kama huwezi kupata usingizi, basi fumba
macho yako na kupumzika kidogo.
Tatu ni kunywa chai kidogo alasiri,
kwani potassium ndani ya mwili wako inaweza kupotea kirahisi katika
majira ya joto, na kunywa chai kunaweza kukusaidia kuhifadhi potassium
mwilini.
Nne ni kulowesha miguu yako ndani ya maji ya moto kila usiku
na kujikanda au kujichua kidogo mwenyewe ambapo itasaidia mzunguko wa
damu mwilini na kusaidia kulala vizuri.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment