Watafiti wa Australia wamepiga hatua katika kuendeleza chanjo dhidi ya ugonjwa wa malaria.
Watafiti
kutoka taasisi ya Walter and Eliza Hall wamegundua njia ya kuzuia
kimelea cha malaria kuvamia chembe nyekundu za damu zenye afya.
Profesa
Alan Cowman aliyeongoza utafiti huo ametoa taarifa akisema, kimelea cha
malaria hakiwezi kupenya katika chembe nyekundu za damu za binadamu
wakati protini muhimu zikiondolewa.
Cowman amesema, ugunduzi huo
unatarajiwa kusaidia kufahamu uwezo wa protini hizo na kuziendeleza kama
chanjo, huku akisema kuendeleza chanjo mpya dhidi ya malaria ni
kipaumble cha utafiti wa kimataifa.
Imefahamika kwamba ugonjwa huo unaua watu hadi laki 4.5 kila mwaka hasa watoto chini ya umri wa miaka mitano.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment