Wanasayansi
wa idara ya utafiti kuhusu usingizi nchini Marekani wamefanya utafiti
kuhusu muda wa kulala unaofaa kwa watoto wenye umri tofauti.
Wamesema muda wa kulala unapungua hatua kwa hatua kufuatia kuongezeka kwa umri wa watoto.
Watoto
wachanga wenye umri wa miezi minne hadi mwaka mmoja wanatakiwa kulala
saa 12 hadi 16 kwa siku, wale wenye umri kati ya mwaka mmoja hadi miwili
wanatakiwa kulala saa 11 hadi 14, umri kati ya miaka mitatu hadi mitano
wanatakiwa kulala saa 10 hadi 13, na umri kati ya miaka 6 hadi 12
wanatakiwa kulala saa 9 hadi 12. Watoto wanahitaji muda wa kulala
usiopungua saa 8.
Wakati binadamu wanapolala, hali ya miili na akili
inafufuka. Kutolala kwa muda wa kutosha kunaongeza hatari ya kupata
magonjwa mbalimbali, yakiwemo kunenepa kupita kiasi, ugonjwa wa
kisukari, na mfadhaiko.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment