Tanzania
itatoa sheria ya kulinda usalama wa taarifa binafsi ili kuimarisha
mapambano dhidi ya uhalifu unaofanyika kupitia mtandao wa Internet.
Hayo
yalidokezwa na naibu waziri wa mambo ya ndani ya Tanzania Bw Yahya
Simba kwenye mkutano wa kilele wa usalama wa Internet unaofanyika Dar es
Salaam.
Bw Simba ameutaja uhalifu kupitia Internet kuwa tishio kuu dhidi ya sekta ya mawasiliano na maendeleo ya watu barani Afrika.
Amesema kupitishwa kwa sheria hiyo kutachangia mfumo wa sasa wa sheria dhidi ya uhalifu kupitia internet.
Mwaka
jana Tanzania ilipitisha sheria ya kupambana na uhalifu wa Internet
ikiwa nchi ya tano kutoa sheria ya aina hiyo ikifuata Kenya, Afrika
Kusini, Nigeria na Zambia.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment