Image
Image

Wakuu wa wilaya mkoani Tanga wala kiapo waaswa kusimamia amani vyema.

Serikali mkoani Tanga imewaagiza wakuu wapya wa wilaya za mkoa wa Tanga kuhakikisha kuwa kamati zao za ulinzi na usalama zinasimamia vyema suala la ulinzi na usalama katika maeneo yao kwa sababu amani inapokosekana shughuli za maendeleo na uwekezaji zitasimama.
Akizungumza na wakuu wapya nane wa wilaya za mkoa wa Tanga baada ya kuwaapisha,Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigella amesema hivi karibuni mkoa wa Tanga utanufaika na ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi katika Bandari ya Tanga hivyo amewataka wakuu wa wilaya ambao bomba hilo litapita wawaeleze wananchi kuhusu fursa za ujenzi wa bomba la mafuta ili waweze kunufaika.
kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akielezea vipaumbele vyake katika nafasi ya ukuu wa wilaya kwanza amemshukuru mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumteua na atahakikisha kero za wananchi zinatatuliwa kwa kushirikiana na wataalama wa Halmashauri ya wilaya ili kero na malalamiko dhidi ya serikali yaweze kutoweka.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment