Akizungumza
juzi kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam wakati wa hafla
ya kuwatunuku vyeti mawakili wapya 624, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed
Chande alisema kwa kawaida jalada ni mali ya mteja, lakini baadhi ya
mawakili hugoma kuyakabidhi kwao wanapoamua kuhamishia kesi zao kwa
wakili mwingine.
“Kazi
hii nayo ina miiko yake, natoa wito kwa mawakili wapya wote kuhakikisha
wanazingatia utaratibu wa kazi zao na kuwa waaminifu kwa wateja wao na
jamii kwa ujumla, huku wakitambua kwamba wao ndiyo msingi wa haki
kupatikana kwa mujibu wa sheria,” alisema Jaji Chande.
Alisema
ongezeko la idadi ya mawakili waliofuzu inaongeza idadi yao nchini
inayofikia 6,424 na inaongeza wigo wa huduma ya kisheria kupatikana kwa
wananchi waishio katika maeneo tofauti nchini. “Hata hivyo, kwa idadi
hiyo bado hatujajitosheleza tukilinganisha na idadi ya Kenya ambao wana
mawakili zaidi ya 14,000 na Uganda 2,500, tunatumaini kwamba wataongeza
uwajibikaji kulingana na taaluma yao na watazingatia maadili,” alisema.
Wakili
Frank Ntabaye ni miongoni mwa waliotunukiwa vyeti, alisema amejiandaa
kuwatumikia wananchi wanaohitaji msaada wa kisheria, hasa katika kesi
zinazohusu migogoro ya ardhi na mirathi.
“Natambua
kuna watu wanaonewa wanakosa haki zao kutokana na kutojua sheria, sasa
kuanzia leo nami nikiwa nimeongeza idadi ya mawakili nchini, nitashiriki
kikamilifu kutoa msaada wa kisheria kwa wale wanaohitaji wakiwamo
wasio na uwezo wa kifedha,” alisema Wakili Ntabaye.
Wakili
mwingine, Happiness Mehena alisema amekusudia kujikita kuwasaidia watu
wenye migogoro ya kifamilia na watoto wanaonyanyaswa kwa kufanyiwa
vitendo vya kikatili.
Kwa
upande wake, Wakili Idd Yassin alisema amejiandaa kuwa wakili wa
kujitegemea ili aweze kuwa na nafasi nzuri ya kujituma katika kusaidia
watu wanyonge kupitia mahakama, wapate haki zao.
Kuhusu TAMBARARE HALISI
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment