Image
Image

Makonda akanusha kutoa kauli ya kuwasaka wasio na kazi maalum nyumba kwa nyumba.

Amesema yeye lake in chini ya Ulinzi na usalama. Aliwaagiza wenyeviti wa mitaa kufanya utambuzi wa watu katika mitaa yao. Najiuliza hivi wenyeviti huwa hawawajui wapiga kura wao?
"Taarifa zilizoenea za kuwakamata vijana wasiokuwa na kazi zimechukuliwa katika namna ambayo sivyo nilivyoteuliwa na Rais wangu Dkt John Magufuli nilifanya mkutano na Wenyeviti wa Mitaa ambao wana mamlaka makubwa sana kwenye mitaa yetu na katika mambo mengi nilioongea nao nilizungumzia suala la ulinzi na usalama wa maeneo yetu nikatoa maelekezo mambo mawili, kwanza wawatake wananchi wao wafahamike kwenye serikali ya mtaa na pili wajue shughuli wanazofanya wananchi wao, mambo haya yanajenga misingi ya usalama na amani katika mitaa yetu, kuwafahamu wananchi wanakupa nafasi shughuli wanazofanya na ukijua shughuli wanazofanya kunakupa nafasi uko salama kiasi gani katika mtaa wako"
"Sijasema wasio na kazi wakamatwe na je ukiwakamata utawaweka kwenye magereza ipi? Lipo kosa la uzururaji una taratibu zake wapo watu nafahamu wapo watu hawataki tu kufanya shughuli na ndio hao hao wanakesha kwenye mitandao ya kijamii wamejipa hiyo kazi kama ajira, hivi unaona raha gani kila siku kutumia 'Instagram' na unamuona alianzisha mtandao huo kila siku anabuni na kuongeza uwezo wa matumizi ya 'instagram' halafu wewe unachekelea kutumia 'instagram' kwa ajili ya vitu visivyofaa, kazi yao ni kubuni magroup ya 'wathsaap', kutengeneza akaunti feki za majina ya viongozi"
Nimeongea na Waziri Mkuu kuona jinsi tunaweza kufanikisha Walimu kupanda mabasi ya mwendo kasi bure. Nia ya Rais Magufuli JP watoto kusoma bure lazima ikamilike. Ndio maana tunapigana kuwaondoa omba omba.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment