WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, amewataka maofisa
uhamiaji waliopo mipakani waache tabia ya kusindikiza wahalifu na wahamiaji haramu.
Amesema kwamba, mtumishi yeyote atakayebainika akishirikiana na watu hao, atachukuliwa hatua za kisheria ikiwamo kufukuzwa kazi.
Mwigulu
alitoa kauli hiyo mjini hapa jana alipofanya ziara ya siku moja mkoani
Kilimanjaro kwa lengo la kujionea njia zisizo rasmi zinazotumiwa na
wahalifu katika wilaya za Rombo na Mwanga.
“Kuna malalamiko
yanawahusu baadhi ya maofisa wa uhamiaji na askari polisi kwamba
wanahusika kuwasindikiza wahalifu wanaofanya biashara za magendo pamoja
na wahamiaji haramu.
“Nawaomba waache mara moja, kama watashindwa, basi wajue watachukuliwa hatua kali pindi watakapokamatwa.
“Ili
kuwabaini watu hao, nakuomba wewe mkuu wa uhamiaji wa mkoa, uhakikishe
maofisa wanaofanya kazi katika mipaka wanafuatiliwa kikamilifu ili
waweze kuchukuliwa hatua kwani wanalichafua Jeshi la Polisi,” alisema
Mwigulu.
Katika maelezo yake, Mwigulu alisema wilaya za Rombo na
Mwanga zinaongoza kwa kuwa na njia nyingi za panya ambazo zimekuwa
zikitumiwa na wahalifu hao.
“Wilaya ya Mwanga ina njia za panya zaidi
ya mia tatu. Rai yangu kwamba njia hizo zidhibitiwe ili kukabiliana na
wahalifu hao sambamba na kushirikisha wananchi.
Akizungumzia suala la kukamatwa kwa wasafirishaji wa wahamiaji haramu
na
kesi zao kuchukua muda mrefu mahakamani, waziri huyo alisema
ameshazungumza na Waziri wa Katiba na Sheria ili kuangalia namna ya
kutatua jambo hilo.
Home
News
Slider
Maofisa uhamiaji waliopo mipakani waonywa watikwa kuacha tabia ya kusindikiza wahalifu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment