Washambuliaji wawili wa kujitoa muhanga wameshambulia katika maeneo tofauti nchini Saudi Arabia jana.
Hakuna
kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo katika kile kinachoonekana
kuwa ni mashambulizi yaliyopangwa na kuratibiwa katika nchi hiyo ya
Kifalme wakati mwezi mtukufu kwa Waislamu wa Ramadhan ukifikia mwisho.
Mmoja
kati ya washambuliaji wa kujitoa muhanga alijiripua karibu na Msikiti
wa Mtume mjini Madina,moja kati ya maeneo matukufu katika dini ya
Kiislamu, na kuwauwa kiasi walinzi wanne.
Mapema jana
Jumatatu,mshambuliaji mwingine wa kujitoa muhanga alijiripua karibu na
ubalozi wa Marekani mjini Jeddah,ambapo alijiuwa na kuwajeruhi walinzi
wawili.
Mshambuliaji wa tatu alishambulia msikiti katika mji wa Washia wa Qatif,lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa.
Saudi Arabia imekuwa lengo la mashambulizi ya kundi la al-Qaeda na lile linalojiita Dola la Kiislamu hapo kabla.
Iran wakati huo huo imeshutumu leo mashambulizi hayo.
Waziri
wa mambo ya kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif amesema hakuna tena
mipaka kwa washambuliaji na Wasunni, na Washia wote wamekuwa walengwa
wa mashambulizi hayo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment