UPANDE
wa Jamhuri katika kesi ya kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni
14 inayowakabili wafanyabiashara wawili, leo unatarajiwa kujibu hoja za
upande wa utetezi ulioiomba mahakama iwafutie washitakiwa shitaka la
utakatishaji fedha.
Washitakiwa katika kesi hiyo ni mfanyabiashara
Mohamed Yusufali “Choma”, aliyewahi kutajwa kuwa anajipatia Sh milioni
saba kwa dakika moja kwa njia ya udanganyifu kutoka katika mapato ya
serikali, na Mkurugenzi wa kampuni ya Northern Engineering Works Ltd,
Samwel Lema.
Washitakiwa walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, juzi na kusomewa mashitaka 222 ya kughushi stakabadhi za malipo
pamoja na nyaraka za kodi ya ongezeko la thamani (VAT) , utakatishaji
fedha na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 14.
Baada ya
kusomewa mashitaka, upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Alex
Mgongolwa uliiomba mahakama ifute shitaka la utakatishaji fedha kwa kuwa
lina mapungufu makubwa ya kisheria ambayo hayawezi kurekebishwa wala
kufumbiwa macho isipokuwa kufutwa.
Alidai ili shitaka liwe la
utakatishaji wa fedha lazima kuwa na dhamira ya kuficha chanzo cha fedha
au lengo la washitakiwa kukwepa adhabu lakini kama hakuna mambo hayo
sheria inatoa mamlaka kwa mahakama kuyafuta mashitaka hayo.
Upande wa
Jamhuri uliiomba mahakama iahirishe kesi hiyo ili wajiandae kujibu hoja
za upande wa utetezi. Hakimu Mashauri alipanga leo upande wa jamhuri
uwasilishe majibu ya ombi hilo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment