Daudi Mwangosi akishambuliwa na askari polisi - Picha iliyopigwa na Marehemu Senga wa Gazeti la Tanzania Daima 2012.
Taarifa
zilizotufikia zinadai kuwa mpiga picha wa gazeti la Tanzania
Daima,aliyepiga picha za tukio la mauaji ya Mwandishi wa Habari wa kituo
cha Channel Ten Daudi ya Mwangosi amefariki dunia.
Taarifa hizo zenye kushtua wanataaluma ya habari pamoja na watu wengine zinajiri ikiwa ni siku moja tu pale ambapo MAHAKAMA Kuu Kanda ya Iringa, KUmhukumu kwenda jela miaka 15 askari polisi Pasificus Simon, kwa kumuua bila kukusudia aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kituo cha
Televisheni cha Channel Ten, Daud Mwangosi, huku picha aliyoipiga
Marehemu Senga ikiwa ndio imeendelea kutumika katika ushaidi juu ya
mauaji ya Mwangosi.
Mwangosi
aliuawa Septemba 2, 2012 eneo la Nyololo wilayani Mufindi mkoani
Iringa, baada ya askari kuzuia mkutano wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema). huku picha pekee ya tukio hilo iliyosambaa ulimweenguni kote ikiwa iliyopigwa na Jemedari JOSEPH SENGA aliyekuwa mpiga picha wa gazeti la Tanzania DAIMA.
"Mwandishi Nguli nchini Tanzania Dotto Bulendu ameandika taarifa hii katika ukurasa wake wa Facebook:
"Simanzi,siku
moja baada ya mahakama kuu kanda ya Iringa kumfunga miaka kumi na
mitano askari ya aliyemuua Daudi Mwangosi,tasnia ya habari yapata
pigo,mpiga picha wa gazeti la Tanzania Daima,aliyepiga picha za tukio la
mauaji ya Daudi ya Mwangosi,SHUJAA JOSEPH SENGA,amefariki dunia usiku
huu.
Senga amefia nchini India alikopelekwa kwa matibabu ya ugonjwa wa Moyo.
Bila
Joseph Senga,shujaa aliyehatarisha maisha yake,akasimama bila
woga,akapiga picha akiwa katikati ya msitu wa askari polisi wenye
silaha,huku anga ikiwa imegubikwa na moshi wa mabomu ya machozi,milio ya
risasi ikisikika,na kuzitunza,zikasaidia kufichua mauaji ya
Mwangosi,leo hii asingekuwa Senga,nadhani kusingekuwa na kesi na mwisho
hukumu dhidi ya aliyemuua Mwangosi.Nakulilia Senga..
Senga,Senga,Senga,Senga,umekwenda,Mungu
aliamua akuweke hai mpaka hukumu itoke na mwisho amekuchukua,Senga
umekwenda wadogo zako katika tasnia tukiwa na hamu ya kujifunza kutoka
kwako.
Senga,Senga,kamsalimie Daudi Mwangosi,mwabie aliyemuua nae
kahukumiwa jela miaka 15,kamwambie mazingira ya waandishi wa habari bado
magumu.
Nenda Senga,picha zako zinabaki kuwa rejea ya mafunzo ya uandishi wa habari katika mazingira hatarishi"
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment