MPIGACHAPA
Mkuu wa Serikali, Cassian Chibogoyo, ametoa mwezi mmoja kwa watu
wanaojihusisha na utengenezaji wa vyeti bandia vya Serikali
kujisalimisha kabla hawajachukuliwa hatua za sheria.
Hivi karibuni
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam liliwakamata watu watatu
ambao walikutwa na vyeti bandia vya kidato cha nne, vyeti vya uuguzi,
stika za Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini
(Sumatra), vyeti vya kuzaliwa na vyuo vya ufundi.
Akizungumza na
waandishi wa habari jana, Chibogoyo alisema wanakusudia kuendesha msako
nchi nzima kuwabaini watu hao na kuwachukulia hatua za sheria.
“Baada ya muda tuliotoa kuisha tutafuatilia mkoa hadi mkoa kuhakikisha tunadhibiti nyaraka bandia,” alisema Chibogoyo.
Aliwataka Watanzania kuacha kutumia vibaya bendera, nembo na wimbo wa taifa kwa sababu ni vielelezo vya taifa.
Alisema
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na ile
inayopendekezwa, zote zinaelekeza kuhusu matumizi bora ya vielelezo vya
taifa kama vile bendera, nembo na wimbo wa taifa.
“Bendera
iheshimiwe, hairuhusiwi kupeperusha bendera iliyotoboka, kupauka au
chafu. Katika maeneo mengine unaweza kukuta bendera inapandishwa au
kushushwa lakini watu wamekaa chini na wengine wanaendelea na shughuli
zao,” alisema Kibogoyo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment