MENEJA
wa kiwanda cha biskuti cha Simba, kilichoko jijini hapa, Suresh
Naranjian Somaiya (72), amekutwa amekufa akiwa na kamba ya kiatu
shingoni.
Somaiya mwenye asili ya Asia na mkazi wa Mtaa wa Barabara
ya Nyerere, mwili wake ulikutwa ukiwa na jeraha dogo upande wa bega la
kushoto, jambo lililosababisha kifo chake kielezwe kuwa ni cha
kutatanisha.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi
alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Julai 9, mwaka huu, saa 10:00
alfajiri katika Mtaa wa Barabara ya Nyerere.
Alisema alikutwa amekufa
kwenye nyumba yake aliyokuwa akiishi na mdogo wake wa kiume, shemeji
yake na msichana wa kazi za ndani (majina yamehifadhiwa).
“Ilipofika
majira ya usiku, mdogo wake huyo wa kiume aliyekuwa anaishi naye,
alipokwenda chooni alimkuta kaka yake akiwa ameanguka na amekufa ndipo
alipotoa taarifa Polisi”, alisema.
Alisema Polisi walifika katika
eneo la tukio na kukuta mwili wa marehemu ukiwa na jeraha dogo begani
ukiwa umefungwa kamba ya kiatu shingoni.
"Tunafanya uchunguzi wa
chanzo cha kifo hicho. Aliongeza kuwa Polisi inawahoji ndugu na jamaa wa
marehemu waliokuwa wanaishi naye. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika
hospitali ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi ”, aliongeza.
Kamanda Msangi aliwataka ndugu na jamaa wa marehemu kuwa watulivu ili Polisi ifanye uchunguzi wake kuhusu chanzo cha kifo hicho.
“ Ikithibitika kuna mtu au watu wamehusika kwenye tukio hili hatua zinazostahili za kisheria zitachukuliwa dhidi yao”, alisema.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment