Image
Image

Serikali ya Tanzania kutokuingia mkataba wa EPA na EAC na EU*Na waziri wa India kuwasili nchini.

Serikali ya Tanzania imesema kuwa haitakuwa tayari kuingia mkataba wa EPA na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na ile ya Juumuiya ya umoja wa Ulaya uliokuwa umepangwa kufanyika tarehe 18 Julai, 2016.
Akizungumza na waandis
hi wa Habari jijini Dar es Salaam Katibu mkuu wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Aziz  P. Mlima ameweka wazi sababu za kutoingia mkataba huo kuwa ni kutokana na kuwa na hofu ya hali ya mambo yalivyo ndani ya umoja wa ulaya ambapo mkataba huo unaweza kufifisha ndoto ya Tanzania ya viwanda.
“Kubwa ni kulinda Maslahi ya kiuchumi ya nchi zetu zenye uchumi mchanga na zenye dhamira ya kujenga viwanda.”Alisema Mlima.
Balozi Mlima ameongeza kuwa madhara makubwa juu ya makubaliano hayo ni uchumi wa nchi changa kugeuka kuwa soko la mataifa yaliyoendelea na kuua viwanda vilivyopo kwa sasa.
Katika hatua nyingine  waziri mkuu wa india anatazamiwa kuwasili nchini  9 Julai, 2016 kwa ziara ya kikazi kufuatia mwaliko wa mwenyeji wake Rais Dkt. John Magufuli ambapo pamoja na mambo mengine ujio huo unatarajia kuzungumzia masuala ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili.


                                                        Balozi Agastino Mahiga
 Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waziri wa mambo ya kigeni wa Tanzania Balozi Agastino Mahiga imesema waziri mkuu huyo wa India anatarajiwa kufika na wafanyabiashara 50 lengo ikiwa ni kuboresha mahusiano ya kibiashara kati ya nchi hizo,ambapo ujumbe huo wa wafanayabiashara utapata fursa ya kubadilishana uzoefu na wafanyabaishara wa Tanzania.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment