Kansela
Angela Merkel atafanya mkutano wake wa kila mwaka na waandishi habari
leo kufuatia mashambulizi kadhaa, ambayo yameitikisa Ujerumani na
kuzusha maswali juu ya sera yake ya kufungua milango kwa wakimbizi.
Merkel alilazimika kukatiza likizo yake ya majira ya joto na anafanya tukio lake hilo la kila mwaka mapema kuliko ilivyopangwa.
Mashambulizi
matatu kati ya manne tangu Julai 18 yalifanywa na watu wanaoomba
hifadhi, na mawili kati ya hayo wanamgambo wa kundi la itikadi kali la
Dola la Kiislamu walidai kuhusika .
Mashambulizi hayo yaliyodaiwa
kufanywa na kundi la Dola la Kiislamu ni pamoja na shambulio na kisu na
shoka katika treni jimboni Bavaria, shambulio la risasi mjini Munich,
shambulio la kisu mjini Reutlingen na shambulio la bomu la kujitoa
muhanga mjini Ansbach.
Umaarufu wa Merkel umeporomoka mapema mwaka
huu kuhusiana na wasiwasi juu ya wakimbizi milioni 1.1 waliowasili
nchini Ujerumani mwaka 2015, lakini ulipanda tena baada ya kura nchini
Uingereza ya kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya mwezi Juni na jaribio la
mapinduzi nchini Uturuki mapema mwezi huu.
Sera kuhusu wakimbizi
Mtu
kutoka Syria ambaye alikuwa anaomba hifadhi ya ukimbizi aliwajeruhi
watu 15 siku ya Jumapili alipojiripua nje ya ukumbi wa tamasha la muziki
katika mji wa kusini nchini Ujerumani wa Ansbach, alikuwa arejeshwe
nchini Bulgaria zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Mashambulizi hayo
yameamsha mjadala juu ya vipi kushughulikia waombaji hifadhi ambao ni
wahalifu na juu ya kuweka ulinzi katika mipaka ya Ujerumani.
Maafisa
katika jimbo la Bavaria, ambako mashambulizi yalitokea, wanatoa wito kwa
wakimbizi kufanyiwa uchunguzi mkali na wa kina pamoja na kubadilishwa
kwa sera ya serikali kutowarejesha wakimbizi walikotoka katika maeneo ya
mizozo.
Merkel amekuwa mara kwa mara akisisitiza kwamba mipaka ya
Ujerumani itabakia wazi na kwamba uhalifu unaofanywa na watu wachache
wanaoomba hifadhi haupaswi kusababisha shaka kwa watu wote ambao ni
wakimbizi.
Makundi ya siasa kali
Ghasia za hivi karibuni zimeleta
msuguano wa kisiasa ndani ya kundi lake la wahafidhina juu ya ahadi yake
ya kuwapa hifadhi wale wote wanaokimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe
nchini Syria.
Kundi la chama cha siasa kali za mrengo wa kulia nchini
Ujerumani la Alternative for Germany, chama mbadala kwa Ujerumani, AfD
limetumia ongezeko la matukio haya ya matumizi ya nguvu kumshutumu
Merkel kwamba anaifanya nchi hii kuwa lengo la mashambulizi.
Kiongozi
huyo wa Ujerumani pia anatarajiwa kuelezea juu ya ghasia zilizotokea
nchini Uturuki kufuatia jaribio la mapinduzi mapema mwezi huu na athari
zake katika makubaliano juu ya wahamiaji kati ya Umoja wa Ulaya na
Uturuki.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment