Rais Barack Obama amewasihi Wamarekani kuacha kukata tamaa kutokana na wasiwasi wa kibaguzi uliojitokeza.
Akizungumza wakati wa misa
ya kumbukumbu ya maafisa polisi watano wa mji wa Dallas waliouawa na
mshambuliaji aliyekuwa akilipiza kisasi mauaji ya watu weusi
yanayofanywa na polisi, amesisitiza kuwa taifa halijagawanyika kama
inavyoonekana.
Rais Obama amekiri kuwa makundi mengi ya watu wachache yamekuwa yakiteseka na ubaguzi.
''.. Marekani, tunajua kwamba upendeleo upo, tunajua hivyo. Aidha uwe Mweusi au mweupe
au Mhispania au M'Asia ama mwenye asili ya kuzaliwa America au
Mashariki ya kati, tumeiona chuki hiyo katika maisha yetu, tumesikia pia
mara kadhaa katika makazi yetu wenyewe...'' alisema Rais Obama.
Lakini
hata hivyo amesema Maafisa wengi wa polisi wamekuwa wakifanya kazi
ngumu na ya hatari na wanapaswa kuheshimiwa, na sio kukaririwa kwamba
wanaupendeleo.
''...Tunajua kwamba maafisa wengi wa polisi wamekuwa
wakifanya kazi ngumu na hatari kwa kuzingatia haki na taaluma,
wanahitaji kupata heshima yetu na sio kudharauliwa. Na mtu yoyote yule
hata kama anania njema, kama atajaribu kuwachafua polisi wote kwamba wanaupendeleo na wabaguzi, kufanya hivyo tutakuwa tunashusha hadhi ya wale maafisa ambao tunawategemea kwa usalama wetu..'' Alisema Rais Obama
Akiwa
njiani kuelekea katika mji wa Dallas, Rais Obama aliwapigia simu ndugu
za Wamarekani weusi wawili waliouawa katika mashambulio ya hivi karibuni
yaliyofanywa na polisi na kusababisha hasira za kufanyika maandamano
nchi nzima.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)




0 comments:
Post a Comment