MAMLAKA
ya Masoko ya Mitaji (CMSA) imeidhinisha ongezeko la ukubwa wa mtaji wa
Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kutoka Sh bilioni 8.25 hadi Sh
bilioni 10.12.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es
Salaam, Meneja Mauzo DSE, Patricki Mususa, alisema kutokana na kuvuka
lengo la mauzo ya awali ya IPO ya hisa zake la kufikisha Sh bilioni 7.0,
DSE imefanikiwa kukusanya Sh. bilioni 35.768 sawa na asilimia 377.
“Mei
16, mwaka huu, DSE iliendesha mauzo ya IPO ya hisa zake ikiwa na
matarajio ya kukusanya mtaji wa Sh bilioni 7.5 kutokana na mauzo ya
hisa bilioni 15 kila moja kwa Sh 500, kufuatia mauzo hayo DSE
imefanikiwa kukusaya mtaji wa bilioni 35.768 sawa na ongezeko la
asilimia 377.
“Utaratibu wa ugawaji wa hisa utakuwa hivi, waombaji wa
hisa zenye thamani ya Sh milioni 5 watapatiwa zote lakini wale ambao
ni zaidi ya hapo watapata hisa sawa na mgawanyo unaoendana na ukubwa wa
maombi na pia watarudishiwa fedha zao kulingana na kiwango cha ugawaji,”
alisema Mususa.
Aidha alisema wafanyakazi wa DSE watapata asilimia 3
ya hisa na kwamba fedha zitakazorudishwa zitakuwa kwa utaratibu wa
hundi pamoja na usajili wa akaunti za CSD utakaokamilika Julai 11, mwaka
huu.
Katika hatua mwingine, Mususa alisema kuwa idadi ya mauzo
katika soko hilo imeshuka kwa asilimia 77 kutoka Sh bilioni 29.1 wiki
iliyopita hadi Sh bilioni 6.6 wiki hii huku idadi ya hisa zilizouzwa na
kununuliwa ikipanda kwa asilimia 113 kutoka milioni 2.5 hadi milioni 5.4
Sambamba
na hilo alisema ukubwa wa mtaji wa soko umeshuka kwa asilimia 0.6
kutoka Sh trilioni 21.0 hadi Sh trilioni 21.7, wakati mtaji wa
makampuni ya ndani ukishuka kwa asilimia 0.9 hadi kufikia trilioni 7.9.
Alisema
makampuni matatu yaliyoongoza kwa idadi ya hisa zilizonunuliwa na
zilizouzwa ni Benk ya CRDB asilimia 66.87, NMB asilimia 18.64 na
kampuni ya bia TOL asilimia 8.72.
“Kiashiria cha sekta ya huduma za
kibenki na za kifedha kimeshuka kwa pointi 86.46 kikiwa kimechangiwa na
kupanda kwa bei ya hisa kwenye kaunta za NMB (1.79%) na CRDB (6.25%),”
alisema Mususa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment