Wizara ya mambo ya kigeni ya China imethibitisha kwamba ndege za kijeshi za China na Japan zilipambana katika eneo la maji linalogombaniwa katika bahari ya Mashariki mwa China mwezi uliopita , na kusema ndege za China zilikuwa zinafanya doria ya kawaida angani.
Wizara
hiyo imesema ndege za kijeshi za Japan zilikaribia ndege za
China kwa kasi kuwachokoza, hali iliyosababisha marubani wa China
kuchukua hatua za kimbinu. Taarifa hiyo iliyotolewa jana Jumatatu haikusema ni hatua gani zilizochukuliwa .
Hali hiyo iliyotokea Juni
17 ilitokea karibu na visiwa kadha vidogo vidogo ambavyo nchi zote
mbili zinadai kuwa ni mali yake, visiwa vinavyoitwa Diaoyu na
China na Senkaku kwa jina la Kijapan.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment