Image
Image

MAJALIWA:Ni Marufuku watu kuvuta shisha nchini Tanzania

                                           KASSIM MAJALIWA- Waziri Mkuu Tanzania.
Serikali imepiga marufuku matumizi ya shisha nchini na kulitaka jeshi la polisi kuhakikisha ulevi huo unatoweka ili kuwalinda vijana ambao ndio nguvu kazi.
Akizungumza kwenye hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na waumini wa dini ya Kiislam madhehebu ya SHIA nchini Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA amesema matumizi ya shisha huwafanya vijana washindwe kufanya shughuli za uzalishaji mali na serikali kukosa nguvu kazi.
Waziri Mkuu MAJALIWA pia amesema serikali itaendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na taasisi za dini nchini za kuhakikisha amani na utulivu unaimarishwa pamoja na kutatua changamoto zinazoikabili jamii.
MAJALIWA amesema katika kuhakikisha amani inakuwepo serikali itaendelea kuimarisha kamati ya amani kuanzia ngazi ya chini ya uongozi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment