Mamlaka ya usafiri wa Majini na nchi kavu (SUMATRA) imeyafungia mabasi 12 ya kampuni ya City boys kutokufanya safari zake kufuatia jana mabasi hayo mawili ya kampuni hiyo kusababisha ajali na kuuwa watu 30 eneo la Manyoni mkoani Singida.
Hatua
hii ni ya awali katika kushughulikia chanzo cha ajali hiyo ambayo
imegharimu maisha ya watu wengi ambapo mpaka sasa madereva wa mabasi
hayo wamekamatwa huku hali za majeruhi zikielezwa kuendelea vizuri na
baadhi yao wamekwisha kuruhusiwa kurejea makwao.
Mabasi hayo mawili ya City boy yaliyokuwa
yakitokea maeneo tofauti moja likitokea Dar-es-Salaam kwenda Kahama na
lingine likitokea Kahama kwenda Dar-es- Salaam, baadhi ya mashuhuda
walisema kuwa mbasi hayo baada ya kukutana yaliwashiana taa na kuanza
kuya yumbisha kama ishara ya kusalimiana na hatimaye kugongana jambo
ambalo linaelezwa kuwa wanafanya hivyo kwa miaka mingi.
Jana Kwa mujibu wa Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida ACP Thobiasi Sedoyeka aliyekuwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo 04 Julai 2016 alisema kuwa ajali hiyo ilisababishwa
na uzembe wa madereva wote wawili kwa kuendesha magari hayo kwa mwendo
kasi na kufanya mzaha Barabarani ili hali wakijua wamebeba roho za watu
ndani ya gari hizo.
Baadhi ya watu mbalimbali wamesikitishwa na hatua hiyo nakusema kuwa kuyafungia tu haitoshi bali madereva hao wapewe adhabu itakayokuwa fundisho kwa madereva wengine wenye michezo hiyo wakati wakiendesha vyombo vya moto.
Home
News
Slider
SUMATRA yayapiga nyundo Mabasi ya City Boys yaliyosababisha ajali na kuuwa Singida kwa muda usio julikana.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment