Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), wameanzisha mfumo wa rejesta ya makazi kwa njia ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama).
Katibu
Mkuu Tamisemi, Mussa Iyombe alisema jana kuwa mfumo huo wa uingizaji wa
taarifa za makazi na wakazi kwa njia ya kielektroniki unalenga kutumia
teknolojia ya kisasa ili kupunguza gharama katika shughuli zake.
“Mfumo
huu utakaogharimu Sh3 bilioni utasaidia Serikali kuwatambua wavamizi na
uwapo wa taarifa ya wakazi wake. Tayari tumejaribu katika Kata ya
Mapinga,” alisema Iyombe.
Pia,
alisema mfumo huo utasaidia kupatikana kwa idadi kamili ya wanafunzi wa
shule za msingi na sekondari, walimu na kiwango cha fedha kinachotakiwa
kutolewa kama ruzuku.
Alisema sehemu kubwa ya fedha hizo itatumika kutoa elimu kwa watendaji wa kata, vijiji na vitongoji kwa muda wa mwezi mmoja.
Alisema baada ya miezi mitatu kutakuwa kukifanyika tathimini kubaini changamoto na mafanikio yaliyopatikana.
Akizungumzia
mfumo huo, Diwani wa Mapinga, Ibrahimu Mbonde alisema mfumo huo ni
mzuri kwani utaleta takwimu sahihi tofauti na awali.
“Mfumo
huu unarahisisha kazi kwani hata kwa simu unaweza kupata taarifa za
mtu, vile vile unaondoa utoaji wa taarifa za uongo na kupunguza gharama
ya kununua vitabu kwani kitabu kimoja kilikuwa na uwezo wa kusajili kaya
50 pekee,” alisema Mbonde.
Kamishna
wa Sensa ya Watu na Makazi, Amina Said alisema mfumo huo huenda ukafuta
utaratibu wa sensa ambayo imekuwa ikigharimu fedha nyingi.
Alisema
fedha hizo zitatumika katika matumizi mengine kwani takwimu muhimu
kuhusu watu na makazi zitakuwa tayari zipo kwenye taarifa.
Kuhusu TAMBARARE HALISI
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment