Waziri wa Mambo ya Ndani Theresa May atakuwa waziri mkuu mpya wa Uingereza hii leo, akiwa na jukumu la kuongoza mchakato wa kujitoa rasmi nchi hiyo katika Umoja wa Ulaya.
Hii ni baada ya mpinzani wake Andrea Leadson kusitisha kwa ghafla kampeni yake ya wadhifa huo.
May
mwenye umri wa miaka 59, atamrithi David Cameron, aliyetangaza kuwa
anajiuzulu baada ya Waingereza mwezi uliopita kupiga kura ambayo
haikutarajiwa ya kujitoa katika Umoja wa Ulaya. Mpango wa Uingereza
kujitoa umeidhoofisha umoja huo wa nchi wanachama 28, kusababisha hali
ya sintofahamu kuhusiana na biashara na uwekezaji na kuyumbisha masoko
ya fedha.
Theresa May na Andrea Leadsom walitarajiwa kupambana katika
uchaguzi wa mashinani wa wanachama wa chama cha Kihafidhina, huku
matokeo yakitangazwa Septemba 9.
akini Leadsom alijiondoa ghafla jana
baada ya kampeni yake kugubikwa na matamshi yaliyozusha utata kuhusu
mpinzani wake kutokuwa na watoto na maswali kuhusu kama alidanganya
katika wasifu wake. Akizungumza baada ya kuthibitishwa kuwa Waziri Mkuu
mtarajiwa, May alisema "Tunahitaji kuiunganisha nchi yetu na tunahitaji
maono mapya, yaliyo bora na imara kwa mustakabali wa nchi yetu. Maono ya
nchi yetu yanayofanya kazi sio tu kwa wachache wanaojiweza, lakini pia
kwa kila mmoja wetu, kwa sababu tutawapa watu udhibiti zaidi wa maisha
yao, na kuijenga Uingereza bora".
Cameron aliwaambia wanahabari kuwa
ataongoza kikao chake cha mwisho cha baraza la mawaziri leo na kujibu
maswali bungeni kesho Jumatano kabla ya kuikabidhi barua ya kujiuzulu
kwa Malkia Elizabeth. May atakuwa waziri mkuu wa pili mwanamke nchini
Uingereza baada ya Margaret Thatcher.
Ushindi wake una maana kuwa
mchakato mgumu wa kuiondoa Uingereza katika Umoja wa Ulaya utaongozwa na
mtu kutoka upande wa kampeni iliyoshindwa. Anasema Uingereza inahitaji
muda wa kuutafakari mkakati wake wa kujiondoa na haipaswi kuwasilisha
rasmi mpango huo kabla ya mwisho mwa mwaka huu.
May alisema katika
hotuba yake jana kuwa hapatakuwa na kura ya pili ya maoni na hakuna
jaribio la kujiunga tena katika Umoja wa Ulaya kupitia mlango wa nyuma.
"Ipo haja ya uingozi thabiti, unaoweza kutuondoa katika wakati mgumu na
usiotabirika wa hali ya kiuchumi na kisiasa. Haja ya kusimamia mpango
bora wa Uingereza kuondoka katika Umoja wa Ulaya, na kujiwekea nafasi
mpya katika ulimwengu. Brexit ina maana Brexit na tutaitumia kupata
mafanikio".
Ikulu ya White House imesema Rais wa Marekani Barack
Obama ana matumaini kuwa “mahusiano maalum” baina ya Marekani na
Uingereza yataendelea baada ya May kuapishwa kuwa waziri mkuu.
Kansela
wa Ujerumani Angela Merkel amesema viongozi wa ulaya watakuwa na
mazungumzo magumu na Uingereza akisisitiza kuwa nchi hiyo haitaweza
kuingia kwa njia huru katika soko la pamoja la Umoja wa Ulaya bila
kukubali uhamiaji huria wa watu.
Naye kamishena wa Uchumi katika
Umoja wa Ulaya Pierre Moscovici amesema mazungumzo yanapaswa kuanzishwa
haraka iwezekanavyo ili kupunguza hali iliyopo ya sintofahamu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment