WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekabidhiwa maabara ya kitabibu inayoweza kubebwa kwenye
sanduku (Mobile and Compact Portable Clinical Laboratory) ambayo ni
rahisi kutumika mahali popote hata kwenye maeneo yasiyo na umeme.
Maabara hiyo ambayo inatumia umeme wa mionzi ya jua inaweza pia kuchajiwa na betri ambayo inawashwa na umeme wa kwenye gari.
Akitoa maelezo mbele ya Waziri Mkuu jana (Jumanne, Julai 12, 2016) ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam,
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya ACCUSTER ya India, Bw. Amit Bhatnagar
alisema maabara hiyo imeundwa kwa lengo la kusaidia kupunguza tatizo la
umbali kwa wananchi waishio vijijini.
“Jumla ya taasisi za kijamii
100 nchini India zimekwishanunua maabara hii na kikubwa wanachojivunia
ni kuweza kuchukua vipimo vya wagonjwa hadi mlangoni kwao kwenye vijiji
zaidi ya 45, wakati mgonjwa halazimiki kutembea umbali mrefu na majibu
anayapata hapohapo,” alisema.
“Kwa wastani maabara hii inaweza
kuhudumia watu 150 kwa siku na kila kipimo kinachowekwa kinatumia muda
wa sekunde mbili kupata majibu yake. Taarifa zake zinaweza kuhamishika
kwa kutumia USB au Bluetooth connection,” aliongeza.
Bw.Bhatnagar
ambaye alikuwa miongoni mwa wafanyabiashata 50 waliombatana na Waziri
Mkuu wa India aliyezuru Tanzania Jumamosi iliyopita, alisema maabara
hiyo ina vifaa vyote muhimu kama Biochemistry Analyzer, Centrifuge,
Incubator, Data Recorder with Patient Data Management Software,
Micropipettes na power back-up. Pia inakuwa na Laptop ndogo ya kupokelea na kuhifadhi taarifa za vipimo vya wagonjwa.
Pia
alimweleza Waziri Mkuu kwamba vifaa vya maabara hiyo vinaweza kufanya
kazi kwenye mazingira yasiyohitaji ubaridi kwani vina uwezo wa kuhimili
joto kuanzia nyuzijoto 00 hadi nyuzijoto 500.
Hata hivyo, Waziri Mkuu ambaye alimwita Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Dkt. Mpoki Ulisubisya aje kushuhudia maabara hiyo, alisema ameguswa
baada ya kubaini kuwa maabara hiyo inaweza kufanya vipimo vingi vikiwemo
vya malaria, magonjwa ya ini, na moyo.
Kwa upande wake, Dkt.
Ulisubisya alimweleza Bw. Bhatnagar kwamba itabidi maabara hiyo pamoja
na vifaa vyake ikafanyiwe uchunguzi juu ya matumizi na kwamba
vikikamilika atapatiwa ripoti kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini
(TFDA).
“Utatakiwa kuandika write-up na kuiwasilisha TFDA na
wakikamilisha uchunguzi, watatuletea taarifa ambayo tutaituma kwako,”
alisema.
Vilevile, Dkt. Ulisubisya alimweleza Waziri Mkuu kwamba ameridhika na wastani wa gharama za vipimo
kwa kila mgonjwa ambayo ni kama sh. 15 lakini bei ya maabara hiyo iko
juu. Awali, alielezwa na Mkurugenzi Mtendaji huyo kuwa bei yake ni rupia
za India 326,000 (sawa na sh. milioni 10.4).
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment