Dar
es Salaam. Ufinyu wa bajeti katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI)
umesababisha taasisi hiyo kuzidiwa na wagonjwa wa upasuaji, huku wengine
wakisubiri huduma hiyo kwa zaidi ya miezi minne.
Kabla
ya tatizo hilo la kifedha MOI ilianzisha kambi maalumu ya Jumamosi na
Jumapili na waliweza kuhudumia wagonjwa hadi 30 kwa siku hizo mbili.
MOI
kwa kawaida hutoa huduma ya upasuaji kwa wagonjwa wanane hadi 10 kwa
siku, lakini kutokana na ufinyu wa bajeti uliosababisha kuondolewa kambi
za mwishoni mwa wiki, umesababisha ongezeko la idadi kubwa ya wagonjwa
wanaohitaji upasuaji.
Uchunguzi
uliofanywa na Mwananchi katika wodi ya MOI jengo jipya, umebaini uwapo
wa idadi kubwa ya wagonjwa waliokaa muda mrefu wakisubiri huduma ya
upasuaji, huku wengine wakirejeshwa nyumbani.
0 comments:
Post a Comment