Ujerumani
inapanga kuomba msamaha rasmi kwa koloni lake la zamani Namibia, kwa
mauaji ya kimbari yaliyofanywa na wanajeshi wa Ujerumani katika nchi
hiyo ambayo wakati huo ilijulikana kama Afrika ya Kusini Magharibi. Hayo
yalitangazwa na wizara ya mambo ya nje mjini Berlin. Wanajeshi wa
Ujerumani waliwauwa watu zaidi ya 75,000 wa makabila ya Waherero na
Wanama kati ya mwaka 1904 na 1908. Ujerumani iliitawala nchi hiyo
kuanzia mwaka 1884 hadi mwaka 1915.
Wizara
ya mambo ya nchi za nje ya Ujerumani imesema mazungumzo kati ya nchi
hizo mbili, ambayo yanayataja bayana mauaji hayo kuwa ya ''kimbari''
yanatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu, na kwamba Rais Joachim
Gauck wa Ujerumani ndiye atakayeomba rasmi msamaha. Ujerumani na Namibia
pia zinanuia kushirikiana katika mipango ya uwekezaji, ukiwemo mradi wa
kuondoa chumvi katika maji ya bahari.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment