ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA), Dickson Maimu na maofisa wengine saba waandamizi, wamepandishwa
kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam
wakikabiliwa na mashitaka 27 yakiwamo ya matumizi mabaya ya ofisi na
kusababisha hasara ya zaidi ya Sh bilioni 1.2.
Washitakiwa wengine ni Mkurugenzi wa Huduma za Kibiashara, Avelin
Momburi, Meneja wa Fedha na Uhasibu, Benamini Mwakatumbula, Meneja wa
Bajeti na Milki, Joseph Makani, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima na
Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond.
Wengine ni Xavery Kayombo ambaye wadhifa wake haukutajwa, na Astery
Ndefe ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers Company
Limited. Washitakiwa hao pia wanakabiliwa na mashitaka yanayohusu
kutumia nyaraka zenye kusudio la kudanganya na kula njama za kutenda
kosa.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage, washitakiwa hao
hawakutakiwa kujibu lolote dhidi ya mashitaka hayo kwa sababu
wanashitakiwa chini ya Sheria ya Uhujumu Uchumi. Wote waliamuriwa
kurejeshwa mahabusu hadi Agosti 31, mwaka huu kesi yao itakapotajwa
tena.
Uchunguzi wa kesi hiyo kwa mujibu wa waendesha mashitaka,
wanaoongozwa na Mwanasheria Mwandamizi wa Serikali, Awamu Mbangwa
haujakamilika. Hakimu alisema kwamba suala la dhamana litaamuriwa na
Mahakama Kuu, kwa kuwa kiwango cha fedha katika kesi hiyo kinazidi Sh
milioni 10.
Lakini alisema atatoa uamuzi kuhusu dhamana kwa washitakiwa Mobuli na
Makani kesho kwa sababu ya hoja kwamba wawili hao hawakabiliwi na
mashitaka ya uhujumu uchumi, kama washitakiwa wengine. Jopo la waendesha
mashitaka linawajumuisha pia Leonard Swai, Janeth Machuria, Joseph
Kiula na Fatma Waziri.
Waendesha mashitaka walidai kuwa katika tarehe tofauti kati ya mwaka
2010 na 2015, wakiwa watumishi wa umma, Maimu na Mwakatumbula walitumia
vibaya madaraka yao kwa kuidhinisha kwa Kampuni ya Gotham International
Limited malipo ya Dola za Marekani milioni 5.175 pamoja na Sh milioni
sita.
Home
News
Slider
Aliyekuwa Mkurugenzi wa vitambulisho ( NIDA )na wenzake 8 wafikishwa Kisutu Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment