ASKOFU
wa Kanisa la Katoliki jimbo la Bunda mkoani Mara, Mhashamu Renatus
Nkwande amewaasa mapadre wasijinufaishe na fedha za mashoga kutoka
nchi za Ulaya katika kuhamasisha haki za mashoga nchini.
Badala yake aliwashauri wajishughulishe na kazi ya kuwakomboa katika dhambi.
Askofu
alisema hayo juzi katika ibada maalum ya kumpa daraja Takatifu la
Upadre, Shemasi Proper Luhinda iliyofanyika katika viwanja vya Parokia
ya Mtume Paulo mjini Bunda.
Alisema ushoga umeanza kuonekana pia mkoani Mara.
Aliwataka
mapadre hao kutekeleza kiapo chao cha utii mbele ya Kanisa na kwa
jamii nzima kwa kupiga vita ushoga na aina zote za dhuluma huku
wakiwahubiri jamii kutunza sheria za nchi na maadili ya Kanisa la
Katoliki.
Naye Mkurugenzi wa miito ya Kanisa hilo Jimbo la Bunda,
Padre Paulo Kamuhabwa aliwataka vijana wa kanisa hilo kujiunga na wito
wa upadre kwa kuachana na anasa za dunia ili waitumikie jamii popote
duniani.
Akisoma kiapo cha utii, Padre huyo mpya aliahidi kutimiza wajibu wake na kuwa na utii na mwadilifu kwa
Askofu wa jimbo hilo, mapadre, watawa na waumini wote.
Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili alilipongeza kanisa hilo kwa utaratibu uliowekwa wa kuwapata mapadre wema.
Alitoa wito kwa waumini wa kanisa hilo kumuunga mkono Rais Magufuli katika kupiga vita maovu nchini.
Mwakilishi Msaidizi wa Baba Mtakatifu nchini Ufaransa, Padre
John
Italuma, aliwataka watanzania kutunza amani iiyopo ili kuepuka ugaidi
kama yanayotokea Ufaransa hivi sasa kwa kuua watu wasiokuwa na hatia.
Padre Prosper Luhinda anakuwa wa kwanza kupata daraja Takatifu tangu Jimbo la Bunda lianzishwe miaka mitano iliyopita.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment