WAKIMATAIFAYanga, jana walishindwa kudhihirisha hilo baada ya kutema
kombe la kwanza kwa kufungwa na Azam kwa mikwaju ya penalti 4-1 katika
mechi ya Ngao ya Jamii iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa uliopo Temeke
(TMK) Dar es Salaam.
Yanga imezoeleka kuitwa wa kimataifa kutokana na uwakilishi wake
kwenye michuano ya kimataifa lakini pia ikipata matokeo mazuri katika
mechi za nyumbani kwa msimu mzima uliopita.
Ikiwa imeshahesabu ushindi baada ya kuongoza kwa mabao 2-1 katika
dakika 90 za mchezo huo, Yanga ilijikuta matatani baada ya Azam
kusawazisha bao dakika ya 90 na kulazimika kwenda kwenye mikwaju ya
penalti baada ya kutoka sare ya mabao 2-2.
Mechi hiyo ni ya kuashiria kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu bara ambayo msimu huu wa mwaka 2016/2017 unaanza keshokutwa.
Yanga imetema kombe hilo ililolitwaa mwaka jana baada ya kuifunga Azam kwa mikwaju ya penalti 8-7.
Timu hiyo bado inashikilia ubingwa wa Kombe la FA na wa Ligi Kuu.
Wachezaji Ramadhan Kessy aliyecheza Yanga kwa mara ya kwanza na
Haruna Niyonzima ndio waliokosa penalti ambapo Kessy penalti yake
kuokolewa na kipa wa Azam Aishi Manula huku Niyonzima kupiga juu. Kipa
wa Yanga Deogratius Munishi ‘Dida’ ndiye aliyepata penalti kwa upande wa
Yanga.
Penalti za Azam zilifungwa na Bocco, Himid Mao, Kapombe na Michael
Balou. Yanga ilianza kwa kasi mechi hiyo na ilionekana kuwa na kila
dalili ya kuibuka na ushindi hasa baada ya Azam kuonekana kutojiweza
karibu dakika zote za kipindi cha kwanza.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Ngoma aliin dikia Yanga
bao la kuongoza katika dakika ya 18 kwa mkwaju wa penalti iliyotolewa
na mwamuzi Ngole Mwangole wa Mbeya baada ya Ngoma kufanyiwa madhambi
eneo la hatari na Shomari Kapombe.
Dakika moja baadaye Ngoma aliandika bao lingine baada ya kuunganisha
krosi ya Amisi Tambwe na kuujaza mpira wavuni. Bao hilo lilizidi
kuwachanganya Azam ambapo sasa wachezaji wake walionekana kupoteana
zaidi lakini walihimili kwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa mabao
hayohayo.
Azam ambayo haikupewa nafasi kubwa kushinda mechi ya jana kutokana na
kukosa matokeo mara kwa mara wanapokutana na Yanga, ilianza kipindi cha
pili kwa mabadiliko ambapo walimtoa Shaaban Chilunda na Ramadhan
Singano na nafasi zao kuchukuliwa na Francisco Zekumbariwa na Mudathir
Yahaya, mabadiliko yaliyoonekana kuzaa matunda kwani sasa ilibadilika na
kuanza kupeleka mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwa Yanga.
Dakika ya 75 Kapombe aliisawazishia Azam bao la kwanza baada ya
kuunganisha pasi ya Jean Mugiraneza na kuujaza mpira wavuni. Dakika ya
90 John Bocco aliisawazishia Azam bao la pili kwa mkwaju wa penalti
iliyotolewa na mwamuzi baada ya beki wa Yanga kushika mpira eneo la
hatari.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment