Mwanariadha
wa Jamaica, Usain Bolt, amefanikiwa kunyakua medali ya pili ya dhahabu
kwenye michezo ya Olimpiki ya Rio, Brazil baada ya kushinda kwenye mbio
za mita 200, ikiwa ni medali yake ya 8 kuinyakua kwenye michezo ya
Olimpiki.
Bolt alikimbia kwa muda wa sekunde 19.78 akimpita Mcanada Andre de Grasse na Mfaransa Christophe Lemaitre.
Muingereza
Adam Gemili alimaliza kwenye muda sawa na Mfaransa Lemaitre, lakini
alishindwa kupata medali yake ya kwanza baada ya mfumo wa picha kutumika
kuamua mshindi.
Botl mwenye umri wa miaka 29, tayari ameshinda mita
100 kwenye michezo ya mwaka huu na anatarajiwa kukimbia kwenye mbio za
mita 4x400 za kupokezana vijiti usiku wa kuamkia Jumamosi.
Katika
hatua nyingine kamati ya Olimpiki ya Marekani imeomba radhi kwa kile
ilichosema tabia isiyokubalika ya waogeleaji wake wa nne ambao
walidanganya kwa kutoa taarifa za uongo wakidai waliporwa mali zao na
majambazi.
Polis iliwahoji waogeleaji hao wa tatu wa Marekani, ambao
baadae walidai kuwa hawakuwa wahanga wa tukio la uporaji kama
walivyoripoti awali.
Wanamichezo wawili kati yao, Gunnar Bentz na Jack Conger waliruhusiwa kusafiri kurudi kwao Alhamisi ya wiki hii.
Mchezaji Ryan Lochte tayari ameondoka Rio na James Feigen bado yuko Brazil.
Kwenye
masumbwi, kiongozi mkuu anayesimamia mchezo wa masumbwi kwenye michezo
ya Rio, amebadilishwa kazi baada ya kukosolewa kutokana na uamuzi wa
majaji na marefa waliosimamia baadhi ya mapambano.
Shirikisho la
kimataifa la mchezo wa masumbwi, Aiba, limesema kuwa mkurugenzi Karim
Bouzidi atapewa majukumu mengine ndani ya taasisi hiyo na nafasi yake
itazibwa na mtu mwingine.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment