Image
Image

DC Songwe apiga marufuku watoto wadogo kujishughulisha na uchimbaji wa Madini.

Mkuu wa wilaya ya Songwe mkoani Mbeya - Samweli Jeremia akisisitiza jambo kuhusu watoto wadogo wanaotumiwa katika shughuli za uchimbaji.
Mkuu wa wilaya ya Songwe mkoani Mbeya Bwana Samweli Jeremia amepiga marufuku watoto wadogo kujishughulisha na shughuli za uchumbaji wa madini katika wilaya hiyo huku akiagiza watendaji wote wa kata kufanya msako wa nyumba kwa nyumba ili kukamata wazazi na walezi ambao wanowatumia watoto wadogo kwa kuwatuma kufanya kazi katika migodi ya madini na kuwaachisha shule.
Mkuu huiyo wa wilaya ametoa agizo hilo katika kijiji cha SAZA wakati akipokea msaada wa madawati 200 kutoka katika kampuni ya Shata Gold Main yenye thamani ya shilingi milioni 23 pamoja kupokea wodi ya wazazi katika kijiji cha mbangala iliyojengwa kwa msaada wa kampuni hiyo ikiwe ni sehemu ya kusaidia jamii.
Aidha Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya saza pamoja na kupongeza jitihada za wadau wa maendeleo kusaidia elimu katika kijiji cha SAZA pia ameoyomba Serikali kufanya jitihada za kuongeza walimu katika shule ya saza kutokana shule hiyo kukabiliwa na upungufu mkubwa walimu hivyo kuchangia kiwango cha taaluma kushuka.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment