Mwanariadha
wa nchi ya Kyrghyzistan, Izza Artykov, amefukuzwa katika michezo ya
Olimpiki inayoendelea katika mji wa Brazil wa Rio de Janeiro, baada ya
kufanyiwa vipimo na kugundulika kuwa alikua akitumia madawa ya kusismu
misuli.
Kutokana na uamuzi huo, Izza Artykov amepoteza medali ya
shaba alioshindia katika kundi la watu wanaopima uzito uliyo chini ya
kilogramu 69.
Uamuzi wa kufukuzwa kwa Izza Artykov umechukuliwa na
Mahakama ya michezo, iliyoombwa kwa mara ya kwanza na Kamati ya Olimpiki
kuhukumu kesi ya matumizi ya madawa ya kusisimua mwili katika hatua ya
mwanzo.
Kyrgyz ambaye alibeba vitu vyenye uzito wa jumla ya kilo 339, alichukua nafasi ya 3 Agosti 10.
Mchina Shi Zhiyong Shi ndiye aliiibuka mshindi, baada ya kumsinda Mturuki Daniyar Ismayilov (kilogramu 351).
Kwa miaka mingi, Izza Artykov alidhoofishwa na matumizi ya madawa ya kusisimu mwili.
Mbulgaria,
amayejulikana kama bibi wa nidhamu amepigwa marufuku kushiriki
mashindano hayo kwa kosa la matumizi ya madawa ya kusisimua mwili.
Wanamichezo
wanane kutoka Urusi waliofuzu kwa mashindano ya Michezo ya Olimpiki
katika mji wa Rio de Janeiro wamewekwa kando kufuatia ripoti ya McLaren
ya Julai 18, inayoonyesha hali ya matumizi ya madawa ya kusisimua mwili
yanayofadhiliwa na serikali.
Agosti 6, mwanamichezo kutoka Cyprus,
Antonis Martasides, alifanyiwa vipimo na kugundulika kuwa alikua kitumia
madawa ya kusisimua mwili, na hivyo kufukuzwa kufukuzwa katika ujumbe
wa nchi yake katika mashindano ya Michezo ya Olimpiki ya Rio de Janeiro.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment